assaph

assaph

Sunday, 28 September 2014

PICHA ZA IBADA YA LEO TAR 28/09/2014

Ibada ya leo ilikuwa na uwepo wa nguvu za Mungu zisizo za kawaida kuwafungua watu mbalimbali waliokuwa wamefungwa.
Add caption

















Sunday, 21 September 2014

IBADA KATIKA PICHA TAR 21/09/2013

Binti aliyekuwa amefanyiwa dawa na kuwa kama zezeta akifanyiwa maombi katika ibada ya leo
Mama huyu akitoa ushuhuda ya matendo makuu ambayo Mungu amemtendea kipindi chote cha uja uzito hadi kujifungua

Binti huyu alikuwa ametupiwa pepo la mauti na alikuja akiwa amebebwa lakini baada ya maombi sasa anaweza kutembea

Pastor Ben akimwombea Haji Mohamed ambae alikuwa hawezi hata kusimama alikuwa amelazwa hospital ya Muhimbili lakini baada ya maombi aliweza kutembea.

Mwl Rachel akifundisha Kipindi cha Alfa

Mama Mchungaji Assaph akimhudumia mtu aliyekuwa na nguvu za giza

Friday, 12 September 2014

ASSAPH MINISTRIES INTERNATIONAL YAANZISHA KANISA DODOMA, WATU WOTE WA DODOMA MNAKARIBISHWA



Huduma ya Assaph ambayo makao yake makuu ni hapa Dar es Salaam itafungua tawi lake jingine huko Mkoani Dodoma, Kanisa hilo litafunguliwa eneo la kisasa ambalo ni makazi mapya kwa wakazi wa mkoa huo, kama ilivyo kauli Mbiu ya Assaph ni Uponyaji wa Yesu kwa Mataifa yote sasa uponyaji huo utawafikia wakazi wa mkoa wa Dodoma na vitongoji vyake. Mchungaji Israel John ambaye ndiye msimamiaji wa kanisa hilo amesema kazi imesha anza na watu wameanza kupokea miujiza yao. Jumapili iliyopita ibada ya kwanza imefanyika huko Dodoma, watu wote waishio Dodoma mjini wanakaribishwa kukutana na nguvu za Mungu zitakazowafanya kuweza kufunguliwa kutoka katika vifungo vyao.
 
Apostle Assaph Benja na mkwewe wabeba maono wa Assaph Ministries
Akiongea kwa njia ya simu alisema kuna mama mmoja ambaye alikuwa anasumbuliwa na uvimbe kwa muda mrefu ameombewa na kutapika finyango za nyama ambazo alilishwa mwaka 90, na kupona kabisa, mama huyo alisema Alisha zunguka kwenye hospital nyingi na alionekana na huo uvimbe ila akipelekwa chumba cha upasuaji uvimbe unapotea lakini kwa jina la Yesu sasa amekuwa mzima kabisa.

Pastor Israel anayesimamia kanisa la Dodoma
 Unaweza kuwasiliana na watumishi hawa kwa no zifuatazo Apostle Ben 0782499991 na watu wa Dodoma Pastor Israel 0786836591