assaph

assaph

Friday, 12 September 2014

ASSAPH MINISTRIES INTERNATIONAL YAANZISHA KANISA DODOMA, WATU WOTE WA DODOMA MNAKARIBISHWA



Huduma ya Assaph ambayo makao yake makuu ni hapa Dar es Salaam itafungua tawi lake jingine huko Mkoani Dodoma, Kanisa hilo litafunguliwa eneo la kisasa ambalo ni makazi mapya kwa wakazi wa mkoa huo, kama ilivyo kauli Mbiu ya Assaph ni Uponyaji wa Yesu kwa Mataifa yote sasa uponyaji huo utawafikia wakazi wa mkoa wa Dodoma na vitongoji vyake. Mchungaji Israel John ambaye ndiye msimamiaji wa kanisa hilo amesema kazi imesha anza na watu wameanza kupokea miujiza yao. Jumapili iliyopita ibada ya kwanza imefanyika huko Dodoma, watu wote waishio Dodoma mjini wanakaribishwa kukutana na nguvu za Mungu zitakazowafanya kuweza kufunguliwa kutoka katika vifungo vyao.
 
Apostle Assaph Benja na mkwewe wabeba maono wa Assaph Ministries
Akiongea kwa njia ya simu alisema kuna mama mmoja ambaye alikuwa anasumbuliwa na uvimbe kwa muda mrefu ameombewa na kutapika finyango za nyama ambazo alilishwa mwaka 90, na kupona kabisa, mama huyo alisema Alisha zunguka kwenye hospital nyingi na alionekana na huo uvimbe ila akipelekwa chumba cha upasuaji uvimbe unapotea lakini kwa jina la Yesu sasa amekuwa mzima kabisa.

Pastor Israel anayesimamia kanisa la Dodoma
 Unaweza kuwasiliana na watumishi hawa kwa no zifuatazo Apostle Ben 0782499991 na watu wa Dodoma Pastor Israel 0786836591

No comments:

Post a Comment