assaph

assaph

Tuesday, 13 May 2014

MAOMBI YA KULIOMBEA TAIFA LA TANZANIA

Tangu Mch Kiongozi wa kanisa la Assaph ministries International aonyweshwe maono ya vita itayo ipata Tanzania kama hakutakuwa na toba na maombi ya kuomba rehema, kanisa limeingia katika maombi ya kuombea nchi.

Akiongoza maombi hayo mama Mch alifundisha andiko kutoka katika kitabu cha 2nyakati 7:14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha , na kuomba na kuutafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na kuiponya nchi yao. Vile alisema tunatakiwa kuwaombea viongozi wa nchi ili wasije ipeleka nchi katika majanga ila Mungu awape hekima na busara katika kuongoza nchi.

Alisoma andiko lingine 2timoth 2:1-2 basi kabla ya mambo yote nataka dua, na sala na maombezi na shukrani zifanyike kwaajili ya watu wote. Kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka tuiishi maisha ya utulivu na amani katika utauwa wote na ustahivu.

Baadae maombi yalifanyika tunahamasisha kila atakae soma habari hii aingie kwenye maombi ya kuombea nchi na washirikishe na wengine. Amen

No comments:

Post a Comment